Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua mfumo wa Kadi wa Kielektroniki wa chama hicho ambao sasa rasmi utaanza kutumika.
Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan amezindua mfumo huo Mjini Musoma mkoani Mara, katika kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama hicho ambacho kimetimiza miaka 45.
Akimkaribisha Mwenyekiti huyo, Katibu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo amesema kuanzishwa kwa mfumo huo ni kuendana na mabadiliko ya teknolojia ambapo utasaidia kuwa na takwimu sahihi za wanachama wao.
Chongolo ameongeza kuwa mfumo huo pia utasaidia kuinua uchumi wa chama hicho kupitia malipo ya kadi hizo.