Jela zakosa chakula Liberia

0
209

Ukosefu wa chakula umeathiri jela zote 15 katika taifa la Liberia na kulazimisha jela mbili kusimamisha kuchukua wafungwa wapya.

Licha ya tajiri mmoja kujitoa kuingilia kati na kusaidia kupunguza uhaba huo lakini matatizo makubwa zaidi yameendelea kutokea ndani jela za nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kujaa kwa wafungwa na ukosefu wa fedha za kuziendesha jela hizo.

Jela kuu iliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Monrovia imeripotiwa kuwa na wafungwa 14,000 ingawa eneo hilo lilijengwa kuweka wafungwa 400 tu.

Hali hiyo imepelekea watetezi wa haki za binadamu kutaka serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua na kuacha kutegemea misaada katika kuendesha jela hizo.