Wafugaji Mkuranga wawezeshwa madume ya ng’ombe

0
180

Wafugaji Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani wawezeshwa na Serikali madume matatu ya ng’ombe aina ya borani ikiwa ni pamoja na kuwakwamua wafugaji hao kiuchumi.

Wakati akikabidhi madume hayo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema madume hayo matatu ya ngombe aina ya borani yatakwenda kuboresha koosafu za ngombe wa asili kwa wafugaji watakao yatumia.

Naye Mkurugenzi wa ranch ya Mbogo, Chalinze Mkoani Pwani, Naweed Mulla ambaye wameshirikiana na Serikali kugawa madume hayo amesema thamani ya madume hayo ni shilingi milioni 15.

“Uzalishaji wa Ng’ombe hawa aina ya borani utasaidia kuboresha koosafu bora ambayo watakuwa bora kwenye uzalishaji wa mazao ya mifugo ikiwemo kiwango kikubwa cha maziwa, nyama, uhimilivu dhidi ya magonjwa na hali ya mazingira ya mikoa yetu” amesema Mulla

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri pia aligawa majokofu 8 kwa vikundi vya wanawake wajasiriamali kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya Uvuvi Ili kusaidia kupunguza upotevu wa ubora wa mazao hayo na kuongeza thamani.