Waziri Ummy Mwalimu ametembelea Zanzibar na kukutana na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Nassor Mazrui na kubadilishana uzoefu kuhusu vipimo vya Corona pamoja na utoaji wa chanjo kisha kutembelea eneo la kupima Covid-19 lililopo Migombani na Uwanja wa ndege wa Amani Abeid Karume.
Ambapo Uwanja wa ndege wa Zanzibar umeweka teknolojia ya haraka ya kupima UVIKO-19 kwa kutumia akili bandia (Artificial Intelligence) ndani ya sekunde moja mtu anaweza kubainika kama ana vimelea au hana.
Zanzibar imepiga hatua katika utoaji wa chanjo kwa wananchi ambapo umefikia asilimia 16 lakini lengo likiwa asilimia 60 ya Wazanzibar wote.