Comoro yaiduwaza Ghana, yaitupa nje AFCON

0
1183

Timu ya taifa ya Comoro imeitupa Ghana nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), baada ya kuichapa mabao 3-2 katika mchezo wa mwisho wa Kundi C usiku wa Jumanne Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua, Cameroon.

Mabao ya Comoro yalifungwa na El Fardou Mohamed Ben Nabouhane dakika ya nne na Ahmed Mogni aliyefunga magoli mawili, dakika ya 61 na 85, wakati ya Ghana iliyomaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Andre Ayew kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 25, yalifungwa na Richmond Boakye dakika ya 64 na Alexander Djiku dakika ya 77.

Matokeo hayo yamewafanya Ghana kutupwa nje kwenye michuano ya AFCON.

Mchezo mwingine wa kundi hilo uliwakutanisha Simba wa milima ya Atlas(Morocco) na Gabon ambapo timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao mawili kwa mawili.

Kwa matokeo hayo Morocco na Gabon wamefuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya kandanda barani Afrika.