Novak Djokovic arudishwa kwao

0
1743

Mchezaji maarufu wa tenisi duniani, Novak Djokovic amesafirishwa kurudi kwao kutoka nchini Australia baada ya maamuzi ya mahakama kukataa maombi yake ya kuendelea kuwapo nchini humo.

Majaji walitupilia mbali pingamizi lililowekwa na mchezaji huyo maarufu ambaye hajachanja baada ya serikali kufuta viza yake.

Matumaini ya mchezaji huyo namba moja duniani kutetea ubingwa wake wa Michuano ya Wazi ya Tenisi ya Australia (Australia Open) na kuweka rekodi ya ubingwa mara 21 yamekwisha.

Djokovic amesema amekatishwa tamaa sana na uamuzi ya hao ila amekubali kuondoka.