Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani kwa wenyeji Ruvu Shooting kutoshana nguvu ya kutoka sare ya kufungana goli moja kwa moja dhidi ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro.
Katika mchezo huo Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa mchezaji Abalkasim Suleiman huku goli la kusawazisha la Mtibwa Sugar likifungwa na Ibrahim Mohamed.
Kwa matokeo hayo Ruvu Shooting wanafikisha alama 11 wakiwa nafasi ya 14 na Mtibwa Sugar ikiwa na alama 11 kwenye nafasi ya 11, wakitofautiana kwa idadi ya magoli.