Sherehe za miaka 58 ya Mapinduzi Zanzibar zafana

0
181

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, leo amewaongoza Wazanzibar katika kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sherehe hizo zilizofanyika katika uwanja wa Amaan, pia zimehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Wengine waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Kilele cha maadhimisho hayo ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar kimepambwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na gwaride maalum lililoandaliwa na vikosi vya KMKM pamoja na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Burudani nyingine zilizopamba sherehe hizo ni ngoma na mashairi.

Kauli mbiu ya sherehe hizo ni Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo Endelevu.

Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12 mwaka 1964.