Waziri mkuu kassim majaliwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya lami kutoka Mbinga kwenda Mbamba Bay yenye urefu wa kilomita 69 itakayogharimu sh. bilioni 129.3 na kuagiza uongozi wa wakala wa barabara tanzania (tanroads) kusimamia vizuri mradi huo.
Waziri mkuu majaliwa amesema hayo mkoani Ruvuma wakati akikagua utekelezaji wa mradi huo wa barabara inayojengwa na kampuni ya Chico ya nchini China na kusema kuwa hatua waliyoifikia inaonyesha barabara hiyo inayotarajiwa kukamilika januari 2021 itakamilika mapema zaidi.
Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutachochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi na mkoa kwa ujumla na kukuza sekta ya utalii na uvuvi katika mkoa huo.