Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi na kupokelewa na Waziri wa Masuala ya Jinsia wa nchi hiyo Patricia Kaliate.
Dkt. Mpango yupo nchini Malawi kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 11 hadi 12 mwezi huu.