Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali, hivyo litaendelea kufanya hivyo pamoja na kumpa Rais ushirikiano.
Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.
Ametumia hafla hiyo kusisitiza kuwa Rais ni Mkuu wa nchi na kwa wale wanaodhani kuwa ni Mkuu wa Serikali waondokane na dhana hiyo, kwani Mamlaka yake ni makubwa na hayafanani na ya kiongozi wa Mhimili wowote nchini.
Kwa upande wa Viongozi walioapishwa, amewataka wakatumie uzoefu wao katika kutimiza majukumu yao ya kila siku na wajitume katika luwatumikia Wananchi.