Timu ya Simba queens imeibuguza bila huruma timu ya Yanga princess magoli 4-1 Katika mchezo uliochezwa Katika uwanja wa Mkapa ikiwa ni muendelezo wa ushindi Katika ligi kuu ya soka la wanawake.
Hadi kufikia mapumziko Simba walikuwa wanaongoza kwa goli Moja na waliporudi wakaongeza goli la pili huku Yanga princess wakipata penati na kufunga goli la kwanza
Simba queens waliongeza kasi na kuongeza magoli matatu ya haraka na kuifanya kuibuka na ushindi wa magoli manne kwa Moja.
Kocha wa Yanga princess Edna Lema amekiri kuzidiwa na Simba Queens na kuahidi kujipanga upya Ili kufanya vizuri kwenye ligi hiyo.
“Nakiri kuwa hatukua na mchezo mzuri leo na mchezo ushapita tunajipanga na mchezo mwingine” Edna Lema
Naye Kocha wa Simba Queens Sebastian Mkomwa amesema walijua watashinda Ila hakujua wangeshinda magoli mangapi japo wanaamini Yanga princess ni timu nzuri na wamecheza kwa tahadhari
“Tunaiheshimu Yanga na tumecheza kwa tahadhari maana tulitegemea kufunga ila hatukujua tutafunga mangapi. Katika kuimarisha kikosi tumeongeza wachezaji wapya naamini wakishika kasi ya wenzao tutafanya vizuri zaidi” Sebastian Mkomwa