Muigizaji maarufu wa filamu za kihindi Salman Khan
Mahakama moja nchini India imemhukumu nyota na muigizaji maarufu wa filamu za kihindi Salman Khan kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua aina mojawepo ya swala ambao ni adimu kupatikana duniani.
Mahakama hiyo iliyoko Jodhpur pia imemtoza nyota huyo faini ya rupia elfu kumi sawa na dola za Marekani 154 kwa kosa hilo.
Khan anadaiwa kuwauwa swala wawili wanaotambulika kwa jina la Blackbucks, ambao hulindwa na kuhifadhiwa, Magharibi mwa Jimbo la Rajasthan.
Muigizaji huyo maarufu wa Bollywood ambaye kwa sasa anaumri wa miaka 52 , anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika mahakama ya juu.