Klabu ya Simba imeuanza mwaka 2022 kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Simba walikuwa wa kwanza kuliona goli la Azam kupitia kwa kiungo kutoka Mali Sadio Kanoute dakika ya 67 kabla ya kiungo mshambuliaji kutoka Senegal Pape Osman Sakho kuongeza goli la pili dakika ya 72.
Dakika ya 79 Rogers Kola wa Azam FC akiandikia bao pekee timu yake, na kupelekea hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi ubao kusomeka 2-1.
Kwa ushindi huo Simba anafikisha alama 24 akiendelea kusalia nafasi ya pili huku kinara Yanga akiwa na alama 29.