Shambulio laua wanajeshi nane

0
198

Wanajeshi Nane wa jeshi la Mali wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa, baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha magharibi mwa nchi hiyo.

Maafisa wa Serikali ya Mali wamesema kuwa, shambulio hilo limetokea karibu na mji wa Nara ulioko katika mpaka wa Mali na Mauritania.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo, ila makundi ya wapiganaji yenye uhusiano na mitandao ya kigaidi yanasadikiwa kuhusika.

Jumatano iliyopita kikosi cha jeshi la Mali kilishambuliwa katika mji wa Niena Kusini mwa nchi hiyo, ambapo hakukuwa na majeruhi.