Rais Samia : Lazima tukope

0
192

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kukopa fedha kutoka taasisi mbalimbali, ili iweze kukamilisha miradi yake mbalimbali ya maendeleo inayoitekeleza.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) awamu ya tatu kipande cha kutoka Makutupora hadi Tabora, Rais Samia Suluhu Hassan amesema hakuna nchini duniani isiyokopa na kwamba hata nchi zilizoendelea zina mikopo mikubwa kuliko Tanzania.

Amesema kamwe Serikali haitavunjika moyo na haitarudi nyuma kutokana na kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kuhusu suala la mikopo.