Polisi kumhoji Nabii Mwingira

0
202

Waziri wa mambo ya ndani, George Simbachawene ametoa maagizo kwa jeshi la polisi nchini kuchunguza na kufuatilia kwa kina tuhuma zilizotolewa na Mtume na Nabii Josephat Mwingira ili sheria ifate mkondo wake

Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa amezipata taarifa hizo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikimnukuu Nabii Mwingira akitoa tuhuma kanisani kwake wakati wa ibada ya Jumapili ikiwemo kutishiwa maisha yake

Aidha, Waziri Simbachawene amesema mtu hawezi kukaa akiwa na hofu na maisha yake hivyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zenye viashiria vya uhalifu mapema kwa jeshi la polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa na kumtaka Nabii Mwingira kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kuthibitisha tuhuma hizo.