Jeshi la Sudan lazima huduma ya intaneti

0
199

Serikali ya kijeshi imedhibiti huduma ya intaneti katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum katikati ya mipango ya kufanya maandamano makubwa ya kupinga mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

Madaraja kadhaa yamefungwa na waandamanaji wameonywa dhidi ya kufanya maandamano na kuleta vurugu katika mji huo.

Wiki iliyopita mamia ya waandamanaji waliandamana katikati ya mji wa Khartoum wakitaka utawala wa kiraia kurudishwa nchini humo baada ya mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 25 mwezi Oktoba.

Wapangaji wa maandamano wanategemea huduma ya intaneti na programu tumishi (App) kupanga maandamano makubwa.

Zaidi ya mamia walijeruhiwa katika mapambano na polisi wiki iliyopita. Vikosi vya usalama pia vilishutumiwa kuwanyanyasa kingono zaidi ya wanawake na wasichana 12.

Wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wanashutumu jeshi la nchi hiyo kuiba mapinduzi ambayo yalipelekea kumwondoa madarakani kiongozi aliyetawala kwa muda mrefu, Omar al-Bashir mwaka 2019.