Yanga yajiimarisha kileleni

0
2435

Klabu ya soka ya Yanga imendelea kusalia kileleni baada ya kuwachapa maafande wa Tanzania Prisons mabao 2-1 kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa.

Mabao ya Yanga yamefungwa na kiungo wake Feisal Salumu dakika ya 23 na Khalid Aucho dakika ya 44 kipindi cha kwanza.

Tanzania Prison ndo walianza kutangulia kwa bao la mapema kabisa lililofungwa na Samson Mbangula dakika ya 12 ya mchezo huo.

Mpaka sasa Yanga anaongoza ligi hiyo akiwa na alama 23 akifuatiwa na Simba wenye alama18 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.