Arsenal yamvua unahodha Aubameyang

0
217

Klabu ya Soka ya Arsenal imemvua unahodha wa timu hiyo mashambuliaji wake Pierre Emrick Aubameyang kutokana na ukosefu wa nidhamu.

Mshambuliaji huyo Raia wa Gabon, ambaye hakuwemo katika mchezo wa Jumamosi ambao Arsenal ilishinda 3-0 dhidi ya Suthampton, pia hatokuwemo katika mchezo wa leo dhidi ya West Ham

”Tunataraji wachezaji wetu wote hususan nahodha wetu, kufuata sheria na viwango vilivyowekwa na kukubalika”, imesema taarifa ya Arsenal.

Hii ni mara ya pili kwa Aubameyang, 32, kuachwa kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kukumbana na adhabu kama hiyo mwezi Machi kutokana na makosa ya ukosefu wa nidhamu