Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) itakutana Desemba 18, 2021 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho kitatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuanzia Desemba 15, 2021.
Taarifa iliyotolewa na katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka imeeleza kuwa vikao vyote ni vya kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 toleo la Mwaka 2020 ibara ya 108 (2). Ambavyo vitafanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma ambapo maandalizi ya vikao hivyo yamekamilika.