Rais awatakia Watanzania heri ya Krismasi na mwaka mpya

0
168

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za heri ya sikukuu za mwisho wa mwaka kwa Watanzania na kuliombea Taifa lisipatwe na maradhi.

Akihitimisha hotuba yake mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba baina ya Serikali na kampuni nne za uchimbaji madini, Rasi Samia amewataka Watanzania kuliombea Taifa na kumuomba Mungu ailinde amani na utulivu uliopo hapa nchini.

“Tukiwa tunaelekea mwisho wa mwaka, niwatakie Watanzania heri ya Krismasi na mwaka mpya, lakini nimuombe mwenyezi Mungu atubariki na kutuondolea maradhi sisi na dunia nzima.” amesema Rais Samia Suluhu Hassan

“Namuomba pia Mwenyezi Mungu alilinde Taifa letu ili amani na utulivu tulionao uendelee kudumu na tuingie salama mwaka 2022.” ameongeza Rais Samia Suluhu Hassan