Wafuasi wa vyama vya ODM na JUBILEE nchini Kenya wameazimia kwa pamoja kumpitisha Raila Odinga kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao nchini humo.
Wakizungumza katika mkutano uliowakutanisha wafuasi wa vyama hivyo kwenye uwanja wa Kasarani, wafuasi hao wamesema Odinga anafaa kuwa kiongozi wa Kenya kwani ana uwezo wa kuwaunganisha Wakenya bila kujali tofauti zao za kisiasa.
Wafuasi wa vyama hivyo wametoa wito kwa Wakenya kuungana na kudumisha umoja na mshikamano, na kupinga ukabila ambao unasababisha mapigano na uvunifu wa amani.
Aidha wafuasi hao wa vyama vya ODM na JUBILEE wamesema kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu ujao unafanyika kwa amani na katika mazingira huru na ya uwazi.
Endapo atapitishwa, hiyo itakuwa ni mara ya tano kwa Raila Odinga kuwania kiti hicho cha Urais nchini Kenya.