Matukio mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru

0
296
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala, akiwasili katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam, yanapofanyika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru.
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo kitaifa ni Rais Samia Suluhu Hassan.


Wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Uhuru uliopo mkoani Dar es Salaam, kushiriki kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru yenye kauli mbiu inayosema kuwa miaka 60 ya Uhuru, Tanzania Imara, Kazi Iendelee.

Miongoni mwa vikosi vinavyoshiriki kwenye sherehe za miaka 60 ya Uhuru zinazofanyika kitaifa katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiwasili katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam kushiriki kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru,
Mgeni rrasmi katika maadhimisho hayo kitaifa ni Rais Samia Suluhu Hassan.


Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam, kushiriki kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja huo.