Waadhimisha miaka 60 ya Uhuru kwa kushiriki ujenzi wa hospitali

0
181

Mkuu wa wilaya ya Songwe, Simoni Simalenga amesema miongoni mwa mambo yanayotakiwa kuenziwa katika miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo Waasisi waliliachia Taifa ni kufanya kazi kwa bidii na kujitoa kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Simalenga ametoa kauli hiyo mara baada ya kuongoza mamia ya Wakazi wa wilaya hiyo kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru kwa kushiriki ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo.

“Katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tunatakiwa kufanya kazi na kujitolea kushiriki miradi ya maendeleo.” ameisisitiza mkuu huyo wa wilaya ya Songwe

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Songwe, Cecilia Kavishe amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaposhirikisha Wananchi unawapa mamlakaya kuimiliki na kuitunza kwa umakini.

Baadhi ya Wakazi wa Songwe walioshiriki katika maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Uhuru wameiomba Serikali kuwajengea barabara ya lami inayotoka Mbalizi mkoani Mbeya kwenda wilayani humo.