Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuweka mipango madhubuti ya kuifanya timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu (Tembo Warriors) kufanya vyema kwenye michuano ya Dunia inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwaka 2022 nchini Uturuki.
Rais pia ameiagiza wizara hiyo kuangalia uwezekano wa kuendelea na kambi ya timu hiyo mpaka mwakani ili kulinda viwango vya wachezaji hao
Aidha Rais Samia ameeleza kufurahishwa na namna wachezaji wa Tembo Warriors walivyokuwa wakicheza kwa umahiri na kuweza kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia hapo mwakani.
Amewataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano yote na kuiletea heshima Tanzania katika medani za soka
Tembo warriors, wamefuzu kuwakilisha Afrika katika fainali za kombe la dunia zinazotarajiwa kufanyika Antalya nchini Uturuki mwezi Oktoba mwaka 2022