Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwala amefunga rasmi mafunzo ya Jeshi la Akiba (mgambo) katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha
Akiwa anakagua gwaride hilo amewapongeza wahitimu kwa uvumilivu mkubwa na nidhamu waliyo onesha kipindi chote cha mafunzo.
Amesema wakufunzi hao walianza wakiwa wengi kwa idadi ya vijana 81 lakini walio hitimu na kupokea vyeti ni 51 tu.
Aidha, mkuu wa wilaya ametoa rai kwa wahitimu na kuwaonya wasitumie mafunzo hayo vibaya bali katika ujenzi wa Taifa na kwa manufaa mapana ya nchi.
“Najua mmefundishwa uzalendo mkawe mfano mwema na mkaonyeshe mmeiva vizuri kwa nidhamu, utii, na unyenyekevu.”
Hata hivyo mkuu wa wilaya ameliagiza Jeshi la Suma JKT kuwachukua wahitimu hao katika majukumu yao sawasawa na uhitaji wao, wasiende mbali wakati kuna jeshi la akiba wilaya ya Ngorongoro.