Rais ateua Ma-DC

0
848

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya.

Said Mohamed Mtanda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi amehamishiwa Wilaya ya Arusha, Abbas Juma Kayanda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu amehamishiwa Wilaya ya Moshi.

Aidha, Rais Samia amemteua Dadi Horace Kolimba, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu. Kolimba anachukua nafasi ya Abbas Juma Kayanda ambaye amehamishiwa Wilaya ya Moshi.