Watumishi 18,000 wahamia Dodoma

0
301

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, zaidi ya watumishi 18,000 wa taasisi mbalimbali za serikali wamehamia Makao Makuu ya Tanzania, Dodoma, ikiwa ni mwendelezo wa kuhamishia makao makuu mjini humo.

Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Jenista Mahagama jijini Dodoma wakati wa uzinduzi awamu ya pili ya ujenzi wa Mji wa Serikali.

Ameeleza kuwa ifikapo mwaka 2023, mji huo utakuwa wa kisasa sana na kwamba katika awamu ya pili wanakusudia kujenga majengo 24.

Katika kipindi cha miaka mitano, Serikali imetumia shilingi bilioni 655.8 katika mambo mbalimbali yanayohusu kuhamia Dodoma, ambapo pia imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 9 ambazo zingetumika kupanga ofisi mkoani Dar es Salaam.

Uamuzi wa kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ulitolewa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi kwa sababu Dodoma ipo katikati ya nchi, jambo ambalo Mhagama amesema limefanikiwa.