Afungwa miaka 42 kimakosa

0
341

Kevin Strickland mwenye miaka 62 ambaye alifungwa kimakosa kwa makosa matatu ya mauwaji mwaka 1978 ameachiwa kutoka jela.

“Sikufikiria siku hii itakuja” , akasema Kelvin kutoka Missouri, Marekani ambaye amesisitiza kwa muda wote Kuwa Hana makosa toka alipofungwa akiwa na miaka 18.

Siku ya jumanne, hakimu aliamuru kuachiliwa mara moja kwa Bwana Strickland baada ya siku 15,487 akiwa jela.

Kulikuwa kifungo kirefu chenye makosa katika historia ya Jimbo hilo, lakini chini ya Sheria ya Jimbo la Missouri inawezakana akakosa kupewa fidia.