Rais awatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 118 wa JWTZ

0
285

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatunuku Kamisheni maafisa wanafunzi 118 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Hafla hiyo imefanyika katika Chuo cha Kijeshi (TMA) kilichopo Monduli mkoani Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wananchi.

Kati ya waliotunukiwa shahada hizo 19 ni wanawake na 99 ni wanaume. Maafisa hao wamehitimu Shahada ya Sayansi Kijeshi iliyotolewa kwa ushirikiano na Chuo cha Uhasibu Arusha, na wengine wamehitimu mafunzo ya Urubani kutoka chuo cha mafunzo Morogoro.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Samia kutunuku kamisheni ambapo Aprili mwaka huu alitunuku kamisheni kwa kundi la kwanza la mwaka 2018 jijini Dodoma na leo ametunuku kundi la pili la 2018.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu pekee ndie mwenye mamlaka ya kutunuku kamisheni, kwani maafisa hao wapya lazima waape mbele yake.

Baada ya kutunukiwa kamisheni maafisa hao wamepews vyeo vya Luteni Usu.

Mbali na Kamisheni, Rais amewatunuku Shahada Sayansi ya Kijeshi wagitimu 61, ambao ni miongoni mwa waliotunukiwa kamesheni.

Akizungumza wakati akifunga mahafali hayo, Rais amewapongeza wahitimu wote pamoja na jeshi, na amewatakia utendaji kazi mwema