Mfahamu mwanamke mfupi zaidi duniani

0
327

Kwa mujibu wa ‘Guinness World Record’ Jyoti Amge kutoka India anendelea kushika rekodi ya kuwa mwanamke mfupi zaidi duniani, Jyoti amezaliwa 16 Disemba 1993), ana urefu wa sentimeta 62.8.

Jyoti Amge alipimwa katika Hospitali ya Wockhardt Superspeciality iliyopo Nagpur India katika siku yake ya kumbukumbu ya kutimiza miaka 18 na kuchukua rekodi hii kutoka kwa Bridgette Jordan ambaye alikuwa anashika rekodi hiyo.

Jyoti Amge hapo awali alikuwa ameshikilia taji la kijana mfupi zaidi (mwanamke) anayeishi ila mpaka sasa Jyoti bado anashikilia rekodi ya mwanamke mfupi zaidi duniani ambayo alipewa 16 Disemba 2011.

Hivi sasa Jyoti ana umri wa miaka 27.