Maduka yateketea kwa moto Mbeya

0
173

Maduka 33 katika Soko la Tunduma yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo wilayani Momba mkoani Songwe.

Mkuu wa wilaya ya Momba Fakii Lulandala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati wa zoezi la kuzima moto.

Lulandala amesema jengo lililokuwa na maduka 43 lote limeungua ambapo katika hayo, maduka 10 yalikuwa hayana kitu na 33 yalikuwa na bidhaa.

Aidha Lulandala amesema chanzo cha moto hadi sasa hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea.