Mbowe na wenzake washinda pingamiza

0
212

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imekataa kupokea kitabu cha taarifa za mahabusu katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam katika kesi ndogo ndani ya kesi ya Msingi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Joachim Tiganga wa mahakama hiyo baada ya kupitia hoja za mawakili utetezi ambao walidai kuwa shahidi wa kwanza ambaye ni miongoni mwa mashahidi 6 kwenye kesi ndogo ndani kesi ya msingi, SP Jumanne Malangahe kwa upande wa Jamhuri alishindwa kuthibitisha kitabu hicho kuwa ni cha Kituo cha Polisi cha Kati cha Dar es Salaam, kupitia mlolongo wa taarifa za mahabusu.

Upande wa jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Mwandamizi Abdallah Chavula waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi la kutopokelewa kwa kitabu hicho kwa madai mawakili wa utetezi wametoa hoja zisizokuwa na msaada wa kisheria hivyo kumlazimu Jaji Tiganga kuahirisha kesi hiyo kwa ajili maamuzi aliyoyatoa leo hii baada ya kujiridhisha na hoja za uetezi na kutupilia mbali pingamizi la upande wa jamhuri.

Hata hivyo mahakama hiyo imesema shahidi SP Jumanne ambaye ni shahidi wa kwanza kwa upande wa jamhuri ameshindwa kukidhi kigezo kimoja cha namna ambavyo kielelezo hicho ambacho aliomba mahakama ikitambue kuwa na taarifa za mahabusu akiwemo Mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Mohamed Ling’wenya kimemfikia baada ya kuachana nacho Agosti 5, 2020.