Uchimbaji gesi asilia nchini kuanza 2025

0
196

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Serikali imeanza mazungumzo na wawekezaji kutoka kampuni ya Equinor na Shell zinazotarajiwa kutekeleza mradi wa uchimbaji wa Gesi asilia kimiminika (LNG) Kusini mwa Tanzania, mradi utakaogharimu shilingi trilioni 70.

Waziri Makmba ameyasema hayo jijini Arusha akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mpaka sasa hatua za awali zinaendelea vizuri hivyo Serikali inatazamia zoezi la uchimbaji wa gesi asilia kuanza ndani ya miaka minne.

Ameongeza kuwa zoezi la uchimbaji na uchakataji wa gesi asilia lilitarajiwa kuanza mwaka 2016, hatua iliyokwamishwa na vikwazo ambavyo kwa sasa Serikali imeweka mipango madhubuti ya kuvitatua.