Wanaojichubua hatarini kupata Saratani

0
225

Tafiti zinaonesha kuwa wanaotumia dawa kubadilisha mwonekano wa ngozi (kujichubua), wapo hatarini kupata ugonjwa wa Saratani ya ngozi kutokana na kupigwa na mionzi ya jua.

Daktari Bingwa wa Saratani, Dkt. Hellen Makwani amezungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano kwa njia ya mtandao (InstaLive) na TBCOnline na kusema kuwa watu wanaotumia vipodozi vya kujichubua wapo kwenye hatari ya kupata Saratani ya ngozi kutokana na kinga ya ngozi kuondolewa.

“Wanaojichubua wapo kwenye hatari ya kupata saratani ya ngozi kwa sababu mtu huyo anakuwa ameondoa melanin kwenye ngozi yake hivyo mionzi ya jua inaweza kuathiri na kupata ugonjwa,” amesema Dkt. Makwani.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi kuweka mazoea ya kuchunguza afya zao ili kuweza kukabiliana na magonjwa endapo yatabainika.