Lukuvi : Hatutaruhusu mtu anunue nyumba nyingi halafu apangishe

0
466

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema wizara hiyo haitaruhusu mtu mmoja anunue nyumba nyingi kisha yeye kuzipangisha kwa wengine.

Waziri Lukuvi amezungumza hayo katika uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa nyumba 1000 kwenye nyumba za makazi zilizopo eneo la Chamwino na Iyumbi jijini Dodoma.

“Hatutakubali mtu aje anunue nyumba 300 halafu yeye ndio ageuke shirika la nyumba kwa kupangisha watu, hilo haliwezekani,” amesema Lukuvi.