Rais Samia kuhutubia Mkutano wa Umoja wa Mataifa Scotland

0
218

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kwenda Glasgow, Scotland kukutana na baadhi ya wakuu wa nchi, wakuu wa mashirika ya kimataifa , wakuu wa taasisi mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi hizo pamoja na Taasisi zao

Rais Samia anatarajia kuondoka kesho kuelekea Scotland kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi
(COP 26)

Aidha katika mkutano huo viongozi wa nchi mbalimbali duniani watajadili kwa kina jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto duniani na kuendelea kutunza mazingira

Katika mkutano huo wa 26 wa Umoja wa Mataifa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhutubia katika siku ya pili ya mkutano huo ambayo itakuwa ni tarehe 2 Novemba 2021