Twiga Stars walamba viwanja

0
328

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya viwanja kwa wachezaji wa timu ya Wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), na kupokea kombe la ubingwa wa COSAFA kutoka timu hiyo Ikulu mkoani Dar es Salaam

Mapokezi hayo yameenda pamoja na hafla fupi iliyoandaliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kula chakula pamoja na Viongozi na Wachezaji wa Twiga Stars ambao wameonesha furaha yao baada ya kukabidhiwa hati za viwanja hivyo vilivyopo mkoani Dodoma

Katika hafla hiyo Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Wanawake nchini kujitokeza na kushiriki katika michezo na kutumia fursa mbalimbali ikiwemo kujiendeleza katika mafunzo ya ukocha

Aidha amesema ataendelea kutoa ushirikiano kwa wanamichezo wote nchini ili kuendelea kufungua fursa za ajira katika sekta ya michezo na burudani.

Rais Samia Suluhu Hassan pia amewataka Wachezaji kuendelea kufanya vizuri na kuitangaza Tanzania na vivutio vya utalii vilivyopo nchini, na wasanii kuendelea kudumisha mila na desturi zilizopo.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema, wamechagua shule 56 ikiwa ni shule 2 kutoka kila mkoa zitakazokuwa kwenye mpango maalum wa kuboreshewa na kujengewa miundombinu ya michezo ili kukuza vipaji katika umri mdogo.