Wananchi Uvinza waaswa kulinda misitu

0
263

Wananchi wanaoishi vijiji vilivyopo mwambao wa ziwa Tanganyika katika Wilaya Uvinza Mkoani Kigoma wametakiwa kutokubali kurubuniwa na watu wasiolitakia mema Taifa kwa kulinda misitu na kuacha tabia ya kukata miti katika misitu ya vijiji vyao

Akizungumza katika kampeni ya Tunza Udongo, Tunza Familia kwa wananchi wa kata ya Sunuka na Sigunga, Afisa Maliasili wa Halmashauri ya Uvinza Daniel Kalabam amesema watu wanaoshiriki vitendo vya kukata miti na kuchoma mkaa kwaajili ya kuuza katika nchi jirani hawapaswi kufumbiwa macho na kusisitiza kuwa kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa maliasili zilizopo kwa ajili vizazi vijavyo

Kalabam amesema kwa sasa afya ya msitu wa Masito Ugala imeteteleka huku misitu ya vijiji ikiangamia kwa kasi na kuhatarisha uhai wa viumbe wanaoishi katika misitu hiyo ili hali misitu ya nchi jirani ikizidi kushamiri.

Kampeni ya Tunza Udongo, Tunza Familia inaratibiwa na Taasisi ya Jane Goodall na inalenga kuhamasisha jamii kulima kwa kutumia Mbolea ya Asili maarufu kwa jina la Mbolea Vunde in