Jaji ajitoa kesi ya Mbowe

0
189

Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mustapha Siyani amejitoa kwenye kesi ya msingi namba 16 ya Mwaka 2021 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Jaji huyo ameeleza kwamba amejitoa kwa sababu ya majukumu aliyonayo kwa sasa, kwamba yatamzuia kuendesha kesi hiyo kwa haraka zaidi kama inavyotakiwa na hivyo kesi hiyo atapangiwa Jaji mwingine.

Baada ya maamuzi hayo washitakiwa wote wamerudishwa rumande mpaka pale Msajili wa mahakama atakapopanga Jaji mwingine atakayendelea na usikilizwaji wa ushahidi wa shahidi wa kwanza Ramadhani Kingai kwa Upande wa Jamhuri.