Mahakama yatupilia mbali pingamizi la Mbowe na wenzake

0
206

Mahakama yatupilia mbali pingamizi za upande wa utetezi la kutaka maelezo ya mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa yasipokelewe, kwa madai yaliwasilishwa nje ya muda wa kisheria na mtuhumiwa alitishiwa kuteswa wakati wa kutoa maelezo.

Mahakama imeridhia kupokea maelezo hayo kuwa kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka

Baada ya uamuzi huo kutolewa na Jaji Kiongozi, Mustapha Siyani sasa ataendelea kusikiliza shahidi wa kwanza kwenye kesi ya Msingi kwa Upande wa Mashitaka, Ramadhan Kingai ambaye hakumaliza kutoa ushahidi wake.