Rais Samia atenga bilioni zitakazotumika kwenye tafiti

0
214

Serekali imeendelea kufanya uwekezaji katika kuboresha na kuwezesha vyuo vikuu na taasisi za utafiti nchini ilikufanya tafiti mbalimbali

Rais Samia Suluhu Hassa amesema serikali imetoa kipaumbele na kwamba kupitia mkopo jumla ya shilingi bilioni 5.1 zimetengwa kufanikisha tafiti mbalimbali ikiwemo zinazohushu UVIKO-19

Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo akiwa Kilimanjaro katika sherehere kuzindua Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC na uwekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Mionzi KCMC

“Ilikuwa na sekta yenye kujibu mahitaji ya wananchi, tafiti ni nguzo imara katika kukabiliana na magonjwa ulimwenguni,” amesisitiza Rais Samia Suluhu Hassan

Pia Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza KCMC pamoja na taasisi nyingine zinzofanya tafiti mbalimbali na kwa kutoa huduma bora kwa weledi.

“Natoa rai kwa wataalamu kuendelea kufanya tafiti mbalimbali za magonjwa na ugonjwa wa UVIKO-19. Nawapongeza wale wote wanaofanya tafiti mbalimbali zinazohusu ugonjwa uliotuvamia wa UVIKO-19 na serekali itaweka uwekezaji Mkubwa katika huduma za Afya, amesema Rais Samia Suluhu Hassan