TPC na DIT kubadilishana uzoefu

0
158

Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeingia makubaliano na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT), yatakayoziwezesha taasisi hizo kubadilishana uzoefu na teknolojia katika usimamizi wa shughuli za kila siku.
 
Makubaliano hayo yataliwezesha Shirika la Posta Tanzania kunufaika na utaalamu wa TEHAMA kutoka DIT, ambao watawezesha mifumo yake ya kuwahudumia Wananchi.
 
Katika Makubalino hayo.  pia DIT watatumia ofisi za Posta zilizopo nchi nzima kutoa mafunzo kwa mafundi kupitia shirika hilo.
 
Mkataba huo wenye vipengele sita unalenga kubadilisha uendeshaji wa Shirika la Posta Tanzania na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam, na kuwahudumia Wananchi kupitia teknolojia ya kisasa popote nchini.