Balozi wa China awasilisha hati kwa Rais Samia

0
206

Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Chen Mingjian, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini.

Rais Samia amempongeza Balozi huyo kwa kuteuliwa kuiwakilisha nchi yake na kumuahidi kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.

Kwa upande wa Balozi Mingjian amempongeza Rais Samia kwa utendaji wake wa kazi na kumuahidi kuimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali hususani biashara na uwekezaji.