Serikali kujenga mizani nyingine Mnazi Mmoja

0
4888

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa muda wa miezi miwili kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi kujenga kituo cha mabasi na malori katika eneo la Mnazi Mmoja,   ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa muda huo mara baada ya kukagua mizani katika eneo la Mnazi Mmoja  lililopo manispaa ya Lindi.

Amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Lindi kujenga mizani nyingine katika eneo la Mnazi Mmoja kwa kuwa mji huo unakuwa kwa kasi na idadi ya magari inaongezeka. 

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Majaliwa, tayari Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mizani hiyo.

Pia amemuagiza Meneja huyo wa TANROADS mkoa wa Lindi kujenga ’round about’ katika eneo la Mnazi Mmoja ili kuwezesha magari ya abria na yale ya mizigo  kuingia na kutoka katika eneo hilo kwa usalama zaidi.