Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameiwakilisha vyema Tanzania alipohutubia Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani.
Amesema kuwa Rais Samia ametoa ujumbe maalum ambao Tanzania ulitaka mataifa mengine yasikie na kuiunga mkono kwenye mipango yake ya maendeleo.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa Septemba 24, 2021) baada ya kukagua maendeleo ya mradi mkubwa wa maji wa Mwanga-Same, Wilayani Mwanga, Kilimanjaro
“Rais ametumia mkutano huo kuyakaribisha mataifa rafiki yenye nia njema ya kuja Tanzania kuwekaza waje. Wito wake huo una manufaa makubwa kwetu,” ameeleza.