Mkoa wa Katavi umepokea zaidi ya shilingi bilioni 15 zitakazotumiwa na Wakala wa Barabara za Vijijiji na Mijini (TARURA) mkoani humo kwa mwaka wa fedha 2021/2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 150 ya bajeti ya miradi ya barabara kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2020/2021 ambapo mkoa huo ulipokea shilingi bilioni 6.1.
Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ametoa taarifa hiyo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Bodi ya Barabara kwa mkoa huo na kuongeza kuwa fedha hizo zitatumika katika kuboresha miundombinu ya barabara iliyopo mkoani humo.