Tusihusishe chanjo na maandiko matakatifu

0
147

Watanzania wametakiwa kutohusisha chanjo na maandiko matakatifu, na badala yake wafuate maagizo ya wataalam wa afya.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Kanisa la Bethany Tanzania, Mathayo Henry wakati wa zoezi la kumsimika askofu mkuu wa kabisa hilo Joshua Isazi lililofanyika jijini Tanga.

“Ni vema tukafuata maagizo ya wataalam wetu wa afya badala ya kupinga na kufananisha chanjo na maandiko. Naamini iko salama maana kama isingekua salama basi viongozi wetu wa ngazi za juu wasingechanja.”

Aidha katika ibada hiyo jumla ya watumishi wa dini wanne walitunukiwa shahada mbalimbali ikiwemo shahada ya uzamivu.

Na Bertha Mwambela Tanga