Waziri Mkuu aagiza kuachiwa kwa Ng’ombe wanaoshikiliwa

0
114

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza mamlaka zote zinazoshikia ng’ombe na mifugo mingine kuachia mifugo hiyo mara moja na warudishwe kwa wamiliki wa mifugo hiyo.

Akijibu ombi la mwenyekiti wa chama cha wafugaji nchini, Jeremiah Wambura, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mifugo na Uvuvi kusimamia agizo hilo la kuachiliwa kwa mifugo hiyo mara moja.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema, mifugo yote ambayo mahakama imeamuru kurudishwa kwa wafugaji basi warudishiwe wenyewe ili waweze kuimiliki na kuendelea na Maisha yao.

Ameongeza kuwa, zaidi ya mifugo elfu 5 imeshikiliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini na hivyo kuagiza mifugo hiyo iachiliwe kuanzia leo na irejeshwe kwa wafugaji.

Hata hivyo amewataka wafugaji kuacha kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyozuiwa ili kuondoa mkanganyiko wa mifugo hiyo kukamatwa kutokana na kuvunja sheria za maeneo husika

Awali akitoa salamu za wafugaji, Mwenyekiti wa chama cha wafugaji nchini Jeremiah Wambura, amemuomba Waziri Mkuu kutoa agizo la kuachiliwa kwa mifugo inayoshikiliwa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini licha ya kuwepo kwa amri za mahakama za kuachiliwa kwa mifugo hiyo.